Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanasayansi vijana wa Tanzania(YST), Dk.Kamugisha Gozibert
Rais mtaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ali Hasani Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa katika sherehe za utoaji tuzo kwa zaidi ya wanafunzi 240 na walimu 120 kutoka mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar waliofaulu katika ugunduzi na utafiti wa kisayansi.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanasayansi vijana wa Tanzania (YST), Dk.Kamugisha Gozibert amesema kazi hizo za ugunduzi na utafiti zinahusisha maeneo mapana ya kisayansi, kazi nyingi zimejikita katika kutafuta ufumbuzi kwa masuala mbalimbali kama afya, kilimo, usalama, mawasiliano na uchukuzi ambayo kwa kiasi kikubwa yanagusa matatizo ya kijamii.
Dkt. Kamugisha amesema utoaji wa tuzo hizo una lengo la kutoa motisha kwa vijana wabunifu na takribani wanafunzi 60 wanatarajiwa kupatiwa zawadi mbalimbali kama fedha taslim, medali, vifaa vya maabara matengenezo ya maktaba na vitabu na wanafunzi sita watazawadiwa udhamini wa kusoma vyo vikuu.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland nchini, Brian Nolan amesema ugunduzi wa kisayansi ni jambo linalotiliwa mkazo na serikali yake na kuwa baadhi ya wanafunzi watakaoshinda watapata nafasi ya kwenda Ireland mapema 2016 kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule za sekondari wanaosoma masomo ya Sayansi Zanzibar wameioba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa elimu mashuleni ya athari za utumiaji wa dawa za kulevya ili kukabiliana na wimbi la ongezeko la vijana kutumia dawa hizo.
Wanafunzi hao wa shule ya Sekondari ya Haile Selasie Fatma Mohamed Nasoro pamoja na Rajab Hemed Mohamed wamesema kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana kuathirika na dawa hizo hivyo serikali iongeze juhudi za kukabiliana na wimbi uingizwaji wa dawa za kulenya visiwani humo.
Wamesema inapaswa watoe elimu kwa wanafunzi wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulenya ambao huwa wanapoteza mwelekeo na kusahau majukumu yao hali inayopelekea kufeli katika masomo ya elimu ya sekondari .