Jumanne , 15th Nov , 2016

Mtoto mchanga wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja Jijini Mwanza amekutwa ametelekezwa kwenye makazi ya watu na mtu asiyefahamika baada ya kujifungua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza, Ahmed Msangi

Tukio hilo limetokea katika  mtaa wa Medical Kata ya Kitangiri ilemela jijini Mwanza  na  mwili wa kichanga hicho umegunduliwa na watoto baada ya kuona kichwa kikiwa nje ya mfuko aina ya  lambo damu zikitoka.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw Patrober Maginga akiwa eneo la tukio amelaani kitendo hicho cha kikatili na kwamba uongozi wa mtaa kwa kushirikiana wananchi watafanya uchunguzi kumbaini  mhusika wa tukio hilo na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Jeshi la Polisi kituo cha Kirumba  Jijini humo wamefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho kwa uchunguzi na hatua zaidi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa, Bw. Patrober Maginga