Jumatano , 28th Jan , 2015

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja amefikishwa leo katika mahakama ya Wilaya ya  Dodoma akikabiliwa na mashtaka mawili tofauti.

Johnson Minja (Kushoto) akiwa mahakamani

Mashitaka hayo ni pamoja na kuwachochea wafanya biashara wa mkoa wa Dodoma kutenda kosa na kuwazuia wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFDs.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Dodoma, Rebeka Mbilu, mwendesha mashtaka wa serikali Godfrey Wambali ameiarifu mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 6/9/2014 katika ukumbi wa chuo cha mipango eneo la miyuji Dodoma mwenyekiti huyo mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Septemba 6, mwaka jana  Mjini Dodoma.

Katika kosa la kwanza mshtakiwa alitenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria namba 390 na katika kosa la pili mshatakiwa alitenda kosa kinyume na sheria kifungu cha 107.

Hata hivyo mshtakiwa alikana makosa yote mawili na alirudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini wawili ambao walitakiwa kuwa na dhamana ya mali ya shilingi milion 4 za mali zisizohamishika ikiwa ni pamoja na mmoja wa wadhamini hao kuwa ni mfanyakazi wa serikali.

Kesi hiyo itatajwa tena Februari 11 mwaka huu.