Jumamosi , 2nd Apr , 2022

Makamu wa rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewaagiza viongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka huu kuhakikisha hawazindui miradi ambayo haiendani na thamani ya fedha iliyotumika huku akiwasisistiza kutoa taarifa za miradi watakayoitilia shaka kwa mamlaka husika ili hatua stahiki zic

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2022

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge mwaka 2022 leo katika viwanja vya Sabasaba, mkoani Njombe huku akisisitiza kuwa Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni kichocheo cha maendeleo na kudumisha umoja na muungano wetu.

“Msizindue kila mradi kutimiza ratiba, hakikisheni miradi mtakayoizindua inaendana na thamani ya fedha iliyotumika, na mtoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwa miradi mtakayoitilia mashaka”  amesema Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.

Aidha Dkt. Mpango ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kukamilisha uchunguzi  wa miradi 52 iliyotiliwa shaka wakati wa mbio za mwenge za mwaka jana 2021, na kuwafikisha mahakamani  waliobainika kuhusika na miradi hiyo.

Dkt. Mpango akatumia nafasi hiyo kuwasisitiza watanzania kuwa tayari kwa zoezi la sensa  ya watu na makazi, linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu huku akibainisha kuwa sense itaisaidia serikali katika mipango wa maendeleo.