Moja ya mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam
Huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka imekuwa ikihudumia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo zaidi ya watu laki moja na nusu kwa siku wamekuwa wakitumia mabasi hayo yaliyoweza kupunguza kero ya wakazi wa Jiji hilo ya kukaa muda mrefu katika foleni barabarani jambo ambalo lilikuwa likisababisha hasara kubwa kiuchumi.
Ni mwaka mmoja tangu usafiri huo kuanza kutumika, Deus Bugarwa ambaye ni Afisa Habari wa UDA-RT amesema huduma ya usafiri itasitishwa kwa muda wa saa 4, kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 7 mchana ambapo ruti za Msimbazi A, Msimbaz B na Terminal Kariakoo zitasimama kwa muda ili kupisha shuguli hiyo ya uzinduzi.


