Akiongea leo jijini Dar es salaam wakati akipokea mashine ya kuchujia maji ya kuoshea vifaa vinavyotumika kwa ajili ya upasuaji, Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo Wilbroda Athanas amesema wanapokea wagonjwa wa nje kati ya 1500 hadi 200 kwa siku huku wagonjwa wa kulazwa wakipokea kati ya 360 hadi 560 huku uwezo ukiwa ni wagonjwa 340 pekee..
Kwa upande wake Victor Manyaga aliyetoa mashine hiyo amesema wameguswa na uhitaji mkubwa wa vifaa tiba walionao wanawake wanaofanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo na kuamua kuchangia.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali hiyo Lusako Evance amesema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa vifaa tiba katika hospitali hiyo hali inayohitaji juhudi za ziada na kupatikana kwa mashine hiyo kutasaidia katika upasuaji.






.jpeg?itok=uqe_Ivr6)