Jumamosi , 29th Feb , 2020

Mwanamke mmoja mwenye umri wa zaidi ya miaka 55, Mkazi wa Kijiji cha Lwemo Kata ya Kagu, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ameibuka katika mkutano wa Mbunge Jimbo la Geita vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) na kutoa kilio chake cha kutengwa na jamii zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Picha si halisi

Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Mbonamengi Mabayi, alitengwa na jamii baada ya kugoma kuhudhuria kwenye msiba wa jirani yake aliyefariki kwa kujinyonga.
 
Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) akataka ufafanuzi wa jambo hilo kutoka kwa viongozi ambapo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Chabwa  Maganga Kaboya akabainisha sababu ya Mwanamke huyo kutengwa na wanakijiji wenzake, na kumueleza Mbunge huyo kuwa suala hilo kwa sasa lipo mahakamani.