Jumatatu , 14th Dec , 2020

Sarah Ngonyani ni mwanamke ambaye aliolewa akiwa na miaka 22, amesimulia namna ambavyo fungate ilivyobadilisha maisha yake kwani mara baada ya fungate ya ndoa yake, mume wake alitarajia kumuona Sarah akiwa ni mjamzito kitu ambacho hakuwa nacho.

Sarah Ngonyani, Mhamasishaji

Sarah amesimulia hayo kwenye kipindi cha MamaMia cha East Africa Radio, na kueleza kuwa ndoa yake ilidumu kwa kipindi cha miezi 18 pekee lakini aliona kama mwaka, kutokana na manyanyaso ikiwemo vipigo alivyokuwa akivipokea kutoka kwa mume wake huyo.

"Niliolewa nikiwa na miaka 22 baada ya kuolewa nilipita kwenye changamoto, kilichotokea mume wangu alitarajia ile miezi ya kwanza baada ya 'Honeymoon' niwe nimeshika mimba, na baada ya hapo tukaanza kupishana yeye anataka mtoto na mimba haitokei, sasa ikawa kama ni mapenzi yaliingilia mlangoni basi yakatokea dirishani", amesimulia Sarah.

Aidha Sarah ameongeza kuwa, "Ikapelekea akawa na hasira na akawa ananipiga mara kwa mara, ikawa hadi kero kwa majirani wakamwambia kama mmeshindwana basi rudishaneni nyumbani, lakini hata baada ya kunioa alikuwa hanipi hela ya nauli ya kwenda chuo, nilikuwa natembea kwa mguu kutoka Mwananyamala hadi chuoni".

Tazama vido hapa chini