Jumatano , 25th Nov , 2015

Mwanamke mmoja mkazi wa Mwanza aliyejifanya daktari amekamatwa katika hospitali ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kwa tuhuma za kutibu wagonjwa kinyume cha sheria.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina Redfrida Garama alifika hospitalini hapo na kuingia katika moja ya chumba cha mganga na kuanza kuhudumia watu waliokuwa wakisubiri huduma kufuatia mganga aliyekuwa katika chumba hicho kwenda katika chumba cha upasuaji ambapo inadaiwa hadi anakamatwa alikuwa tayari amekwisha hudumia takribani watu kumi.

Mganga mfawidhi katika hospitali ya wilaya ya Kibondo Dk. Kizito Luhanja alisema walipewa taarifa na hivyo kumkamata na kumhoji kwakuwa hawamfahamu na sio mtumishi wao.

Hata hivyo mganga huyo alisema mwanamke huyo amepelekwa katika katika vyombo vya sheria ili kufanyika uchunguzi kutokana na yeye kukiri kuwa kitaaluma ni mtumishi wa afya.

Hata hivyo baadhi ya wagonjwa katika hospitali hiyo wamelalamikia huduma mbovu inayotolewa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa vipimo maalumu pamoja na wataalam wa afya.