Bi Stela Juma (Bibi wa mtoto) akiwa amembeba mtoto aliyetelekezwa na mama yake
Msichana wa mwenye umri wa miaka 25 Bi Tausi Hamisi anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa chuo kimoja kilichoko Karatu ambaye ni mkazi wa Magugu Wilayani Babati mkoani Manyara ametaroka hosipitali baada ya kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa mdomo na kichwa huku ubongo wake ukiwa nje.
Mtoto huyo mwenye umri wa wiki mbili ambaye kwa sasa analelewa na bibi yake ambaye ni mama wa mume wa msichana huyo bi Stela Juma akisaidiana na dada wa baba wa mtoto huyo bi Eliza Charles ambao wameiomba serikali na wasamaria wema kumsaidia mtoto huyo.
Aidha walezi wa mtoto huyo wamesema kabla ya tukio hilo mschana na kijana huyo walikuwa wanaishi pamoja eneo la Moivaro Tengeru wilayani Arumeru mkoa wa Arusha na alipoanza kuumwa alipelekwa hosipitali ya wilaya ya Tengeru na kufanyiwa upasuaji wa mtoto huyo.
Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Dkt Azizi Msuya amesema walilazimika kumfanyia upasuaji mschana huyo baada ya kubaini kuwa mtoto alikuwa na matatizo sehemu ya kichwa na alitolewa salama.
Dr Azizi amefafanua kuwa wazazi wa msichana huyo walipofika na kumuona mtoto huyo walitoroka na ndipo akabaki na mama wa baba wa mtoto na baada ya tukio hilo walimhamishia hosipitali ya mkoa kwa msaada zaidi
Kwa yeyote atakayeguswa na awasiliane na bibi wa mtoto huyo kwa namba 0762684005 au afike ofisi za ITV Arusha au awasiliane na Bwana Asraji Mvungi kwa simu namba 0767510326