Kijana huyo amechukua maamuzi hayo baada ya wazazi kumhoji kwa tuhuma walizozipokea toka kwa majirani ambapo walimtuhumu kwa wizi wa fedha katika kibanda cha Nyumbani kwao pamoja na kutohudhuria masomo shuleni.
Akizungumza kwa niaba ya Familia baba mkubwa wa Marehemu Fadhiri Mwamlima amesema kuwa usiku wa tarehe 10/9/2024 wazazi walimuita kijana wao kumhoji juu ya matukio ya wizi wa hela kwenye kibanda chao ndipo kijana alikiri kuwa na chenji alizodai anaenda kuzichukua ili awaletee na baadaye walisikia kelele kutoka jikoni.
Amesema walipotoka walikuta kijana amejichoma kisu na utumbo uko nje na walipojaribu kumkimbiza hospitali kijana alifariki akiwa njiani. #EastAfricaTV