Jumatano , 9th Nov , 2016

Zaidi ya watu 40 hawana mahali pa kuishi mara baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba 32, ofisi ya kata na mahakama ya mwanzo katika kijiji cha Ruanda, Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge.

 

Akizungumza katika eneo la tukio lililokubwa na kadhia hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge ameitaka kamati ya maafa kufanya tathmini haraka ili kujua ni watu wangapi wanahitaji msaada wa haraka.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa mkoa huo kujenga nyumba zilizo imara zaidi ili kuepuka majanga kama hayo yasiweze kuwakumba hasa wa wakati wa mvua kama hizo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amemshukia kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma na kusema amechelewa kutoa taarifa kwa kuchukulia suala hilo ni jambo dogo na kumtaka awasiliane na ofisi yake pindi matukio kama hayo yanapojitokeza.

Nao waathirika wa majanga hayo wameiomba serikali kuwapa msaada ikiwemo mabati ili waweze kujihifadhi hususani katika kipindi hiki cha mvua za masika.