Jumatano , 6th Jan , 2016

Kaya zipatazo 150 wilayani Tandahimba mkoani Mtwara hazina makazi kufuatia upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha kwa muda mfupi unaokadiriwa kutozidi dakika 3 katika vijiji vya cha Chaume na Sokoine na kuezua nyumba.

Mbali na nyumba kuezuliwa, upepo huo piaumesababisha nyumba nyingine kubomolewa vibaya huku baadhi ya wakazi wakikosa chakula.

Wakizungumza baada ya tukio hilo badhi ya waathirika wamesema mvua hiyo licha ya kuezua paa na kubomoa nyumba pia iliangusha miti ya mikorosho, na kuharibu vyakula vilivyohifadhiwa ndani.

Waathirika hao wameziomba kampuni, watu binafsi, mashirika mbalimbali kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu ambacho wanakabiliana nacho.

Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmad wa chama cha CUF amesema mara baada ya kupata taarifa za tukio hilo aliwasiliana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Luhaula ambaye kwa haraka aliwasiliana na kamati yake ya ulinzi na usalama ambayo iliwahi kufika eneo la tukio kwa ajili ya kujua ukubwa wa maafa.