Tundu Lissu akiwa na Spika Ndugai.
Musukuma ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 7, 2019 bungeni jijini Dodoma baada ya kuomba mwongozo wa Spika.
"Lissu anazunguka huku anasemekana anaumwa, ni lini Bunge litasitisha mshahara wake kwa sababu ameshapona na ameendelea kuzunguka huko na huko akitukana Bunge na serikali," amehoji Musukuma.
Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai amesema suala hilo linahitaji kuangaliwa kwa upekee. "Jimboni hayupo, bungeni hayupo, nchini hayupo, hospitali hayupo na mimi sina taarifa yoyote wala ya daktari".
Hoja yako ina msingi iko haja ya kusimamisha mishahara wake," amesema Ndugai na kuahidi atayafanyia kazi mambo yaliyo ndani ya uwezo wake.
Lissu yupo ziarani nchini marekani ambapo ni muendelezo ya ziara yake barani Ulaya, ambapo pamoja na ziara hiyo amedai kuwa bado yupo chini ya uangalizi wa daktari hivyo atakaporuhusiwa atarejea nchini.





