Ijumaa , 3rd Jun , 2016

MKOA wa Mtwara umepiga hatua katika vita vya kupambana na ugonjwa wa Malaria na kufanikiwa kupunguza maambukizi mapya kutoka asilimia 33.6 mwaka 2010/2011 mpaka kufikia asilimia 17 kwa tafiti zilizofanywa mwaka jana.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,

Akizungumza mkoani humo wakati wa kupokea mwenge wa Uhuru kutoka mkoani Lindi, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amesema mapambano hayo bado yanaendelea na lengo ni kufikia chini ya asilimia Moja au sifuri.

Aidha, amesema mkoa unaendelea kupambana na maambukizi ya Ukimwi ambapo mwaka 2010 maambukizi yalikuwa ni asilimia 5.6 kabla ya kupungua mpaka kufikia asilimia 4.1 kwa takwimu za mwaka huu.

Ukiwa mkoani Mtwara, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua jumla ya miradi 40 katika halmashauri zote tisa na wilaya tano za mkoani humo yenye thamani ya sh. Bilioni 49.8 huku mchango wa wananchi ukiwa ni sh. Bilioni 1.8 katika fedha hizo

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,