Alhamisi , 30th Oct , 2014

Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kigoma, wawili wakituhumiwa kukamatwa na meno ya tembo katika wilaya ya Kasulu na mmoja akituhumiwa kumuua kwa kumkata panga mtoto wa miaka miwili katika wilaya ya uvinza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed

Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kigoma, wawili wakituhumiwa kukamatwa na meno ya tembo katika wilaya ya Kasulu na mmoja akituhumiwa kumuua kwa kumkata panga mtoto wa miaka miwili katika wilaya ya uvinza.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed, amesema katika tukio la kwanza wakazi wa kijiji cha Nyakitonto wilayani Kasulu Benjamin Charles na Thadeo Simon wametiwa mbaroni baada ya taarifa za raia wema kufanyiwa kazi na jeshi la polisi lililopekua nyumba zao na kuwakuta wakiwa na nyara za serikali.
 
Katika tukio la pili, mkazi wa kijijim cha Kandaga  Henry James, anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumuua kwa kumkata panga shingoni mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka miwili ..