Jumanne , 27th Aug , 2024

Binti mmoja anayefahamika kwa jina la Halima Mohamed amelazimika kuhamia Dar kwa ajili ya kufanya kazi za ndani ili aweze kuwasaidia wadogo zake wanne ambao mama yao aliwatelekeza baada ya kupata mume mwingine.

Halima Mohamedi binti aliyetelekezewa wadogo zake

Anasema mama yao aliwaacha na baba yao lakini baadae baba yao akapata kesi ya kumbaka mtoto wao na hatimaye kufungwa gerezani.
"Wakati mama ametukimbia baba alikuwa anaenda kumuomba mama wasaidiane malezi lakini mama alimwita baba msumbufu hivyo atampoteza haikupita muda mrefu mdogo wangu alibakwa na aliyedaiwa kufanya hivyo alikuwa baba wakati tukio linatokea mimi sikuwepo kwahiyo sijui ni nani aliyetekeleza tukio hilo hatimaye baba akafungwa", alisema Halima Abdallah, Binti wa kazi.

Kutokana na ugumu wa maisha ikamlazimu kuja Dar es Salaam, kwa ajili kupata fedha zitakazomsaidia kuwalea wadogo zake 4 huku akiomba msaada kwa Serikali.
"Naiomba Serikali inisaidie kwanza wadogo zangu waweze kusoma lakini pia wapate makazi kwani, nyumba niliyowaacha haina usalama wa kutosha lakini ilinibidi niondoke sikuweza kubaki kuwaangalia wadogo zangu wanalala na njaa ingali nina nguvu za kufanya kazi nahitaji wadogo zangu wasome waweze kuondokana na umaskini uliosababisha leo tunateseka", alisema Halima Abdallah, Binti wa kazi.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii kiongozi, Waziri Nashiri anasema ofisi za ustawi zimekuwa zikiwajibika katika malezi ya watoto wakati taratibu za kisheria zikifanyiwa kazi.
"Inapotokea mzazi ameteleekza mtoto cha kwanza tunashauri akafun guliwe Kesi Polisi na sisi ustawi tunawajibika katika malezi ya watoto hao mpaka pale atakapopata walezi au watapelekwa kwenye vituo vya ustawi vinavyotambulika", alisema Waziri Nashiri, Afisa Ustawi Kiongozi Jiji la Dar es Salaam.

Aidha anatoa wito kwa jamii kuhusu malezi ya watoto yanayoweza kupelekea ukatili.
"Mlinzi wa kwanza wa mtoto ni mzazi wake sasa mzazi anapokuwa anakwepa majukumu yake anasababisha mtoto kukutana na ukatili kwahiyo niihamasishe jamii na wazazi kushirikiana klwa pamoja kwenye malezi ili kuepusha kizazi kisicho na malezi bora", alisema Waziri Nashiri, Afisa Ustawi Kiongozi Jiji la Dar es Salaam.