Jumanne , 21st Jun , 2016

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mhe. Edward Ngoyai Lowassa ameitaka serikali kutoa uhuru kwa vyama vya upinzani kueleza hoja zao badala ya kuzuiliwa huku akieleza kuwa anaunga mkono jambo wanalofanya wabunge wa vyama vya upinzani kudai Demokrasia.

Mhe. Lowassa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa vyakula vya futari na kuwatakia Ramadhani njema watoto waliopo katika vituo vya watoto Yatima vitatu Jijini Dar es Salaam ambavyo ni UMRA, CHAKUWAMA, na HYARAT.

Mhe. Lowassa amesema pia kitendo cha kuingiliwa kwa shughuli za kisiasa wanazofanyiwa vyama vya upinzani sio sahihi kwani ni cha kuminya demokrasia, huku akitaka wapinzani waachwe wafanye shughuli zao kwani hazijavunja amani.