Jumapili , 9th Jan , 2022

Baada ya kuibuka kwa mitazamo tofauti baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiuzulu, tumemtafuta aliyekuwa Spika wa Bunge kuanzia 1994 hadi 2005 Pius Msekwa kwaajili ya ufafanuzi.

Msekwa ameeleza kuwa taratibu zote zimefuatwa na hakuna kilichoharibika kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

''Spika amechaguliwa na bunge, kwahiyo utaratibu sahihi barua ya Spika kujiuzulu ni lazima ipelekwe kwenye bunge na isomwe ndani ya bunge''  Spika Mstaafu Pius Msekwa ametoa ufafanuzi.

Zaidi msikilize hapa