Jumatatu , 17th Feb , 2025

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye alifanya mgomo wa kula wiki iliyopita, amekimbizwa hospitalini baada ya afya yake kuzorota, Besigye ambaye anajulikana kama mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni amekuwa kizuizini katika kituo cha usalama katika mji mkuu Kampala tangu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye alifanya mgomo wa kula wiki iliyopita, amekimbizwa hospitalini baada ya afya yake kuzorota, Besigye ambaye anajulikana kama mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni amekuwa kizuizini katika kituo cha usalama katika mji mkuu Kampala tangu Novemba mwaka jana.

Mawakili wake wanasema "alitekwa" katika nchi jirani ya Kenya ambako alikuwa amesafiri na kusafirishwa kwa nguvu hadi Uganda, ambako alishtakiwa katika Mahakama Kuu ya Jeshi kwa makosa mbalimbali yakiwemo kumiliki silaha kinyume cha sheria.

"Dkt. Besigye ameletwa kliniki katika kituo cha Bugolobi Village Mall na ulinzi mkali" Francis Mwijukye, mbunge anayeshirikiana na Besigye, amsema katika chapisho lake kwenye jukwaa la X Jumapili jioni.