Alhamisi , 4th Aug , 2022

Moja ya ghala la kuhifadhia vifaa vya ujenzi la kampuni ya MAN Construction, lililopo maeneo ya Mikocheni viwandani linateketea kwa moto mchana wa leo Agosti 4, 2022, ambapo hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Moja ya kontena lililoteketea

Kwa mujibu wa mashuhuda, moto huo umeanzia katika moja ya kontena la vifaa vya magari, kwani kampuni hiyo pia inajihusisha na utengenezaji wa magari.