Alhamisi , 10th Nov , 2016

Moto mkubwa umetokea kwenye ghala la vipuli vya magari na matairi la Saba General lililopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni shoti ya umeme.

Moto ukiteketeza ghala hilo

Moto huo umeteketeza matairi ya pikipiki, baiskeli na matairi ya magari yaliyokuwa yamehifadhiwa katika ghala hilo.

Moto huo ambao umeonekana kuwa mkubwa umeanza majira ya saa sita na nusu mchana ambapo gari saba za vikosi mbalimbali vya zima moto na uokoaji vilikuwa vikionesha jitihada za kuuzima moto huo na hadi EATV inaondoka katika eneo hilo saa nane na robo mchana moto huo ulikuwa bado haujazimwa.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda amesema hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa au kufariki kutokana na moto huo hivyo taarifa rasmi itatolewa mara baada ya kuzimwa kwake