Ijumaa , 27th Nov , 2015

Mtu mmoja ambaye hajajulikana aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Mark II grande yenye namba T 183 AVT, amefariki dunia baada ya gari hilo kuteketea kwa moto.

Kwa mujibu wa kamanda mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Pwani SSP Abdi Issango, amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo imetokea leo majira ya saa 12 :30 alfajiri maeneo ya Kidimu Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo dereva wa gari hiyo alikuwa kwenye mwendo kasi hivyo kushindwa kukata kona na hatimaye kugonga mti na kupelekea gari hiyo kuwaka moto.

Kamanda Issango amesema masalia ya marehemu huyo yamepelekwa kwenye hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha na kuhifadhiwa hapo.