Jumatatu , 28th Nov , 2022

Mganga mkuu mkoa wa Morogoro Kusirye Ukyo amesema  mkoa huo umeweka malengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa asilimia hamsini huku akieleza kuwa mkoa huo  unashika nafasi ya tano kwa vifo hivyo nchini 

Amesema sababu kubwa ya vifo hivyo imetajwa ni akinamama kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua pamoja na kifafa cha mimba huku watoto wakishindwa kupumua baada ya kuzaliwa

Ameyasema hayo katika mkutano ambao umefanyika wilaya ya Kilosa na kuwakutanisha wa madakta bingwa, madaktari wa vituo vya umma, binafsi, na mashirika ya dini mkoani hapa, kwa ajili ya kutengeneza mwarobaini wa kuondoa vifo hivyo

Kutokana na changamoto hiyo ya vifo vya akina mama na watoto  mkuu wa wilaya ya kilosa bwana Majid Mwanga akifungua mkutano huo wa madaktari amesema elimu inatakiwa kutolewa kwenye jamii juu namna ya kuzuia vifo vya akina mama na watoto visitokee