Akizungumza na waandishi wa habari katika Taasisi hiyo Dkt bingwa wa mifupa Mechris Mango, amesema kwamba mfumo huo utawezesha taarifa kufika kwa urahisi katika chumba hicho maalumu, na kufanyiwa tafsiri itakayowawezesha madaktari waliotuma X-ray hizo kufanya maamuzi wao wenyewe.
"Madaktari wakiwa kule kwenye mashine za X-ray, wanatuma picha ambazo zinasafirishwa kwa njia za kidigitali,na zikishafika hapa sisi tutaziona na tunaweza kuzifanyia tafsiri ambayo itamuwezesha Daktari aliyeituma kufanya maamuzi" .amesema Dkt Mango.
Aidha Taasisi hiyo itakuwa ikitoa huduma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, watakaowezesha huduma hiyo kupatikana kwa urahisi zaidi.




