Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Sara Msafiri Ally.
Hatua hiyo ni baada ya mkuu wa wilaya ya Hanang Sarah Msafiri kuiagiza halmashauri ya wilaya kufanya tathmini upya ili kulilipa kanisa lililojenga kimakosa katika eneo la shule.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Saidiel Isango amesema kuwa ni muhimu kufuata taratibu husika ili kupata muafaka wa jambo hilo ambapo mwenyekiti huyo amesema kuwa suala la mgogoro katika jamii halihitaji siasa kwa ajili ya kuleta maendeleo
Samuel Lyimo ni afisa ardhi wa wilaya hiyo ambapo naye ameeleza kuwa serikali ya kijiji pamoja na wajumbe wake waweke wazi kuhusu sakata hilo ili kuweza kufahamu undani wa suala hilo.
Mara baada ya majadiliano hayo ndipo mkuu wa wilaya ya Hanang, Sara Msafiri Ally akahitimisha kwa kuiagiza halmashauri ya wilaya kufanya tahmini ya ujenzi na gharama za kanisa lililopo eneo la shule ili kumlipa fidia mchungaji wa kanisa ndani ya siku 20.