Akitangaza uamuzi huo wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani lililokutana kujibu hoja za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, CAG, Mkuu huyo wa Mkoa, amesema, licha ya kusimamishwa kazi, hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, Bi. Dendego amewaagiza baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo walioshirikiana na wanasiasa kutafuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya uuzwaji wa viwanja hivyo kuzirudisha fedha hizo mara moja.
"Wapo viongozi waliokula pesa na ushahidi ninao Hakuna wa kupewa kiwanja kiholela hapa. Najua wao waliotafuna pesa hizo na saizi tunazungushana hapa Watapike pesa za watu walizokula" Bi Halima Dendego.
Msikilize hapa chini akizungumza Bi Dengego