Jumatatu , 20th Apr , 2015

Jeshi la Polisi Zanzibar jana limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF, waliokua wakikaidi amri ya kutotoka Wilaya moja kwenda Wilaya nyingine kuhudhuria mkutano wa hadhara.

Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Hamad.

Hali hiyo inakua baada ya Mkutano wa Polisi na vyama vya Siasa kukubaliana na marufu ya wafuasi wa chama kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine kuhudhuria mkutano kwa sababu za Kiusalama.

Akihutubia wananchi katika mkutano uliofanyika eneo la Kilombero Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Hamad amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kuweka vizuizi kila kona ya eneo la mkoa huo ili wananchi washindwe kuhudhuria mkutano huo.

Aidha alilitaka jeshi la polisi kutoa ufafanuzi juu ya sheria iliyotumika kuwazuia wananchi kuhudhuria kutoka wilaya moja kwenda nyingine akisema kitendo hicho kinazuia uhuru wa watu kuhsiriki shughuli za kisiasa.

Aidha alilishauri jeshi hilo kuzingatia hali ya Uchumi na Mazingira ya Zanzibar kwani kitendo hicho cha kuweka vizuizi barabarani kinaleta Taswira mbaya kwa wageni na kinaeza kuhathiri hali ya uchumi ikizingatiwa Zanzibari inategemea zaidi sketa ya utalii.