Jumatatu , 3rd Oct , 2016

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amewalaumu watu waliokuwa wakifanya fujo, kwa kusababisha mkanyagano katika jimbo la Oromiya, ambako amesema watu 52 wamefariki dunia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Amekanusha ripoti kwamba, vikosi vya jeshi vimefyatua risasi katika tamasha la kidini lililokuwa likihudhuriwa na mamia kwa maelfu ya watu.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema ghasia zilianza wakati waandamanaji walipo ingilia kati hotuba za maafisa katika tamasha hilo katika mji wa Bishoftu.

Upinzani nchini humo unasema takriban watu 100 wamekufa. Wengi wa watu hao, walikufa baada ya kuangukia kwenye korongo, wakati wakijaribu kukimbia.