Jumanne , 27th Sep , 2022

Wizara ya maliasili na utalii nchini imezindua mkakati wa kukuza na kutangaza vivutio vya utalii nyanda za juu kusini kupitia mradi wa kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii wa kusini ikiwa ni jitihada za kuendelea kuboresha sekta ya utalii

Waziri wa  maliasili na utalii Balozi Dr.Pindi chana amesema kwa sasa wizara inaendelea na uboreshaji wa miundombinu katika vivutio vya utalii kupitia mradi wa Regrow lengo likiwa ni kuimarisha vivutio vyote vya utalii kusini mwa tanzania.

Mkakati huo umeshirikirikisha mikoa Tisa ya kusini mwa Tanzania ambapo wakuu wa mikoa hiyo kwa umoja wao wameahidi kutoa ushirikiano kwa wizara katika kuhakikisha wanaboresha na kutangaza vivutio vya utalii.

Uboreshaji wa vivutio unalenga kupanua wigo katika wizara ya utalii ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Wakati jitihada hizo zikifanyika mkoa wa njombe umeomba uboreshaji wa uwanja wa ndege ili uweze kutumika huku wananchi wakitakiwa kutoa ushirikiano katika kutuza vivutio hivyo