Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda .
Pinda ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Dodoma ambapo amesema wakati fulani kwenye uongozi wake wapinzani waliwahi kusema serikali yao ni dhaifu haina makali hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uthubutu.
"Wakati fulani kuna baadhi ya watu huwa wananiuliza hivi mzee na wewe si ulikuwa unautaka urais nawajibu tu aka huyu huyu ndiye anayefaa, mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana JPM." amesema.
Amesema chini ya Rais Magufuli serikali imefanya baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, mradi wa kuzalisha umeme wa Stigler’s Gauge na Serikali kuhamia Dodoma.
"Si kwamba tulikuwa hatujui tunatakiwa kuhamia Dodoma ila utekelezaji wake ndiyo uliokuwa mgumu kwa sababu kila ukitaka kuhamia unakuta hakuna maji, barabara bado hazijajengwa na miundombinu mingine kwa hiyo unajikuta unaendelea tu kusubiri mpaka muda wako unaisha bila mafanikio," amesema.
Mizengo Pinda ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne alikuwa ni miongoni mwa makada waliojitokeza kutaka kupewa nafasi ya kuwania urais wa Uchaguzi Mkuu 2015 ambapo Rais Maguli aliibuka kinara.