
Licha ya ongezeko hilo kuwa na fursa nyingi ambazo zinaweza kumsaidia kijana kujiongeza kiuchumi,na wakati mwingine kuburudika baadhi ya mitandao imekuwa ikianzishwa kwa ajili ya kukusanya taarifa za inteliejensia kwa ajili ya mataifa yao.
Kupitia kipindi cha Supa Breakfast imezungumza na mtaalam wa mitandao na Mkurugenzi wa Jamii Forum Maxence Mello anasema baadhi ya mitandao hii baadhi yao huanzishwa kwa lengo la kukusanya taarifa za watu na kutumia kwa matumizi yao lakini zaidi ni kwa ajili intelijensia .
Mitandao mingi ambayo inaanzishwa sasa hivi mgfano Threads, TickTock na mengine inakusanya taarifa na taarifa hizo zinasaidia sana kwenye Intelijensia ya mataifa ambayo inatoka mitandao huyo,na kwa bahati mbaya watumiaji wa mitandao wamekuwa watumiaji tu na hawajali taarifa wanazoweka lakini ukienda kwenye kifaa chako cha simu inarekodi sauti yako muda wote hata kama huutumii na kuchukua baadhi ya taarifa zako
Mello ameeleza pia tahadhari na hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kuhakikisha taarifa binafsi za mtu hazichukuliwi na mitandao hiyo .
Jambo la kwanza kujua mitandao hukimbilia picha zak,sauti yako na pia kuangalia kama mtandao unakuruhusu kujiondoa ukiona haukupi fursa ya kujiondoa kuwa makini , mfano kama Threads ni ngumu sana kujiondoa
Lakini mwisho amemaliza kwa kusema kuwa kila ujio wa mitandao ambao unakuja una Fursa nyingi muhimu ni kuelelewa na kuuliza wataalamu wa maeneo hayo ili kufahamu fursa halisi ilipo