
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahindi wanaojishughulisha na na viwanda(IPF)Gagan Gupta kushoto na muwakilishi wa CHICO Guo Zhijian mapema leo ofisini kwake.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea msaada wa zaidi ya shilingi milioni 40 zilizotolewa na makampuni mawili tofauti, Mhe. Majaliwa amesema misaada yote ya vyakula na vifaa vya ujenzi itapelekwa yote Bukoba na kugaiwa kwa walengwa.
Akizungumzia shule za mbili za Ihungo na Nyakato ambazo majengo yake yameharibika kutokana na tetemeko la ardhi Kagera na kupelekea shule hizo kufungwa Mhe. Majaliwa amesema wamepata wafadhili ambao wamejitokeza kuzijenga.