Ijumaa , 4th Jan , 2019

Rais John Pombe Magufuli amemtaka Kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba kuwaondoa viongozi wote ambao wanakwamisha utekelezaji wa mambo mbalimbali ndani ya NFRA.

Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 04 Januari, 2019 wakati wa kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

''Usiogope kwa wale mchwa waliokuwepo usijali umri wao wala kukaa kwao wewe watoe na wale ambao huna uwezo nao mwambie Waziri au Naibu Waziri wako na wale mnaofikiri mpaka mimi niambia nitawatoa kesho hawatakuwepo'', amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais ameongeza kuwa NFRA inatakiwa ipunguze gharama za oparesheni kwasababu zikiwa juu kila siku itakuwa inapata hasara kutoka kwa wanao nunua nafaka.

WFP kupitia kwa Mkurugenzi Mkazi wake hapa nchini Bw. Michael Danford, imetia saini kununua tani 36,000 za mahindi kutoka NFRA zenye thamani ya shilingi Bilioni 21.