Kitale ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV, na kuongeza kuwa yeye kama msanii hua anajituma kwa hali na mali na kuweza kufanya vitu ambavyo vipo kila siku katika jamii lakini kwa lengo la kuchekesha watu.
''Mimi hua naigiza vitu hivi hivi ambavyo vinatokea katika jamii kila siku sema mimi nachukua na kuweka katika namna ambayo kila mtu akisikiliza au kutizama lazima acheke'' amesema Kitale
Aidha Kitale amewashauri wasanii wenzake wa kuigiza na kuchekesha kuhakikisha kuwa wanakuwa na mawazo tofauti kama wanavyofanya wanamuziki na sii kuigiza kitu kimoja kila siku na kwa aina moja ya muonekano jambo linalowafanya mashabiki kuwachoka.






