
Zaidi ya shilingi milioni 770 zimebainika kulipa watumishi hewa mkoani Mbeya baada ya Idadi ya watumishi hewa waliogundulika mkoani humo kuongezeka kutoka 68 hadi 170.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani humo mkuu wa mkoa wa Mbeya Amosi Makala alisema awamu ya kwanza ya uhakiki wa watumishi hao walibainika 68, na walipoamua kufanya uhakiki upya ndipo idadi ilipoongezeka mpaka kufikia 170.
Aidha Makala alisema kuwa kati ya watumishi hao hewa watumishi 58 walikuwa wamekopa shilingi milioni 480 kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha.
Alizitaja halmashauri zilibainika kuwa ni Rungwe watumishi 28,Chunya 28, Mbarali 30, Busokelo 20, Jili la Mbeya 21, wilaya ya Mbeya 26 na Halmashauri ya Kyela 26.