Ijumaa , 18th Mar , 2016

Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatarajia kutumia shilingi milioni 400 ili kuviwezesha vikundi vya vijana kuanzisha shughuli za uzalishaji,adhima hiyo inafuatia agizo la rais la kuwasaidia vijana kuweza kujiajiri au kuajiriwa.

Kushoto ni Naibu Meya Jiji la Mwanza, Katikati ni Mstahiki Meya na Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza

Wakizungumza Jijini Mwanza baadhi ya vijana Mkoani humo amesema matokeo ya vijana wengi kushinda vijiweni ni pamoja na ukosefu wa mitaji, Masharti magumu ya mikopo, pamoja na mifumo mibovu ya halmashauri kuwasaidia vijana.

Kutokana na Changamoto hizo zinazowakabili vijana hao, Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeamua kutenga fungu maalumu la milioni 400 ikiwa ni mpango wa kwanza wa kuwasaidia vijana takribani 200.

Aidha halmashauri hiyo imetoa wito kwa vijana watakaofaidika na fedha hizo waweze kuzielekeza katika shughuli za uzalishaji kwa kuwa uzoefu unaonyesha vijana wengi huwa wanashindwa kujiendeleza kwa fedha hizo za mikopo kwa kuendekeza starehe.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire, amesema kuwa Halmshauri hiyo imetenga maeneo 11 kwa ajili ya wafanyabiashara Ndogondogo sambamba na Ujenzi wa soko kubwa la kisasa ili vijana wengi wapate sehemu ya kuendeleza mitaji yao.