Jumatatu , 26th Aug , 2024

Kesi ya watu kuripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha mkoani Singida imeendelea kuchukua sura mpya baada ya miili ya watu watatu kuripotiwa kuuwawa kwa imani za kishirikina.

Jeshi la Polisi limetoa mwendelezo wa taarifa yake iliyotolewa Agosti 24 mwaka huu ya kukamatwa kwa watu watatu ambao ni Selemani Nyandalu, Saidi Haji na Nkamba Kasubi ambae ni mganga wa kienyeji  waliohusishwa katika mauaji hayo 

Watu hao wamelionyesha Jeshi la polisi mahali walipo wafukia watu hao akiwemo Samwaja Sifaeli Saidi ambae walimuuwa na kukata sehemu zake za siri.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza Agosti  24, 2024 mashimo mawili yalibainika ambapo baada ya kufukuliwa ulipatikana mwili wa Gideon Samweli mkazi wa makuro mkoa wa singida ambae mara ya mwisho alionekana amepakiwa kwenye pikipiki Octoba 15 2023, na taarifa za kutoweka kwake kurIpotiwa polisi na mwili mwingine uliokuwa haujatambulika ila ni mabaki ya mwili huo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza chanzo cha Gideon kuuwawa ni kitendo chake cha kuuza shamba mara mbili kwa wateja tofauti ambao ni Hawa Mohamedi na Idi Hussein wakazi wa Singida ambao wateja hao mara baada ya kugundua hivyo walifikisha jambo hilo kwa mganga wa jadi ambapo aliambiwa ili fedha yao irudi watahitajika kutoa kafara