Jumanne , 18th Feb , 2025

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 40 amehukumiwa kifungo cha miaka 150 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua watoto wake watatu mnamo 2019 katika eneo la Lelaitich, kaunti ya Bomet.

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 40 amehukumiwa kifungo cha miaka 150 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua watoto wake watatu mnamo 2019 katika eneo la Lelaitich, kaunti ya Bomet.

Wakati akitoa hukumu hiyo Jumatatu, Jaji wa Mahakama Kuu ya Bomet Julius Kipkosgei Ng'arng'ar alipitisha hukumu hiyo huku kila kesi ikiendeshwa kwa miaka 50 mfululizo.

Benard Kipkemoi Kirui alipatikana na hatia ya kuwaua wanawe watatu; Amos Kipngetich (12), Vincent Kiprotich (8) na Emanuel Kipronoh (5yrs) wakati mama yao alikuwa mbali na nyumbani.

Jaji Ng’arng’ar alitaja mauaji hayo kuwa ya kikatili na yasiyo ya kibinadamu, na kwamba adhabu hiyo itakuwa mfano kwa wengine wenye nia ya kutenda uhalifu kama huo. Hata hivyo, mtuhumiwa amepewa siku 14 za kukata rufaa.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuwaua wanawe watatu mwanaume huyo alijaribu kujitoa uhai kwa kujinyonga, lakini kamba ilikatika.