
Tundu Lissu
Akisoma mashtaka hayo mwendesha mashtaka Wakili Paul Kadushi amesema Kosa hilo walilitenda kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka huu katika maeneo ya Dar es salaam baada ya kuchapisha gazeti lenye kichwa cha habari kilichosomeka “Machafuko yaja Zanzibar” katika gazeti la Mawio chapisho namba ISSN 1821 696X no. 182 tarehe 14th January 2016.
Hatahivyo mheshimiwa Tundu Lisu akuweza kufika mahakamani hapo yeye na mshtakiwa mwingine ambaye ni mwandishi wa habari hiyo ndugu Jabir Idrisa Yunus na kulazimu mahakama hiyo kutoa hati ya wito kwa washtakiwa hao.
Watu wengine waliofunguliwa shitaka hilo ni ndugu Simon Makina ambaye ni muhariri wa gazeti hilo, Ismael Mehboob ambaye ni mchapishaji wa gazeti hilo.
Naye wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala amesema mahakama hiyo aina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo inayohusu masuala ya Zanzibar, pia ameiomba mahakama kuwafutia kesi wateja wake kutokana na mashitaka mengine kukosa idhini ya kimaandishi ya mwendesha mashitaka DPP.