Muonekano baada ya kutokea Ajali ya gari Mwaka jana katika kijiji cha Changarawe wilayani Mafinga mkoani Iringa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imezindua mkakati wa kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani zinazosababishwa na mwendo kasi, ulevi, rushwa pamoja na kutozingatiwa kwa sheria.
Akizindua mpango huo, leo jijini Dar ee salaaam Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amesema, mkakati huo utadumu kwa miezi sita ukilenga kuyashughulikia mambo 26 yanayochangia ongezeko la ajali za barabarani.
Mhandisi Masauni ameongeza kuwa, katika mkakati huo, madereva walevi, askari wanaopokea rushwa watawekwa rumande mara baada ya kubainika na makosa, wakati serikali ikiangalia namna ya kurekebisha sheria za usalama barabarani zilizopitwa na wakati





