
Kushoto ni mbunge wa Buchosa Eric Shigongo na kulia ni Spika wa Bunge la 12 Job Ndugai
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 27, 2021, Bungeni Dodoma, kwenye mkutano wa 3 kikao cha 17, wakati akiwasilisha ripoti ya kamati ya kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira.
"Mh. Spika naomba nichukue nafasi hii kukupongeza kwa namna ambavyo umewaletea heshima kabila la wagogo kwa sababu huko nyuma mimi nilikuwa najua kazi ya wagogo ni moja tu kukaa kando ya barabara na kuuza maji", amesema Shigongo
Aidha ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa namna ambavyo ameanza kuihudumia nchi huku akiwaomba wanaume wote kuwaunga mkono akina mama.