Pichani ni Mgombea ubunge jimbo la Musoma Mkoani Mara kupitia chama cha, ADC, Ernest Ojung'a.
Mgombea huyo wa ubunge ameyasema hayo hii leo na kudai kuwa anakabiliwa na ukosefu wa fedha za kuendeshea kampeni jambo ambalo linampa wakati mgumu wa kunadi sera zake kwa wananchi ambapo anaimani akifanikiwa kufanya kampeni wananchi wataweza kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo la Musoma.
Ojung'a amesema fedha hizo ambazo anaomba kwa wananchi zitamsaidia kufanya kampeni kwani amekuwa akitumia baiskeli kupita mtaa kwa mtaa.
Hata hivyo mgombea huyo kwa tiketi ya ADC amesema moja ya sera yake ni kufufua viwanda vilivyopo katika jimbo la Musoma ili kuwezesha ajira kwa vijana na kuwasaidia wajasiriamli wadogo.