
Wananchi walioonekana kuwa na jazba kwa madai kuwa viongozi wa wilaya hizo walipanga kufanya mkutano na wananchi kuhusu mgogoro huo lakini ghafla wamebadilisha na kuwaita viongozi watano wa mila katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha na viongozi wa mila walikataa lakini baadaye mkuu wa wilaya ya Longido James Ole Milya alifika kwa wananchi hao na kuwaeleza walichopanga ndipo wanawake wa kimasai wanye jazba wakaanza kumrushia maneno na kutaka kumfanyia fujo.
Wananchi wa vijiji vinavyo husika na mgogoro huo wamesema wakati umefika wa kwenda kuwaona viongozi wa kitaifa kwa kuwa dalili zinaonesha kuwa viongozi wa Wilaya na mkoa wameshindwa kutatua kwa madai ya kumpendelea mwekezaji huku aliyewai kuwa mbunge wa Monduli na mkuu wa wilaya mbalimbali nchini Lepilali Ole Mureimet akidai kuwa kuna kila dalili za rushwa katika jambo hilo.
Kwa upande wake mwekezaji anayelalamikiwa na wananchi Peter Johns amedai kuwa hana tatizo na majirani zake kwani kampuni yake inasaidia masuala mengi katika vijiji hivyo na kutoa ajira kwa vijna lakini kuna wachochezi wachache wanao sababisha mgogoro.