Mgambo wa almashauri wakielekea kufungua Mageti mara baada ya kukubaliana na Mkurugenzi wa Jiji.
Wakizungumza na chombo hiki mgambo hao wa jiji la Mbeya wanadai kuwa wameamua kufikia hatua hiyo ya kufunga mageti kutokana na kukaa siku 90 bila kulpwa fedha zao huku wakiendelea kufanyishwa kazi.
Kaimu mkurugenzi jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro, amekili kuwepo kwa changamoto hiyo ya mgambo kutolipwa fedha zao muda mrefu na kudai kuwa taratibu za kuwalipa zinafanyika kwani mufumo wa malipo ndiyo uliokwamisha.
Hali hiyo ya mgambo wa jiji kufunga mageti wakidai pesa zao za mishahara imeungwa mkono na baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya.
Kutokana na hali hiyo wakazi wa jiji la Mbeya wameongeza kuwa ni vema serikali ya halmashauri ya jiji la Mbeya ikawalipa mgambo hao pesa zao ili kumaliza mvutano uliopo.