Jumanne , 12th Jul , 2016

Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali umeongezeka kwa asilimia 9.3 katika mwezi june kutoka asilimia 8.2 mwezi mei.

Wananchi Kisiwani Unguja wakiwa katika harakati za kupata mahitaji katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Unguja,

Ofisa Mwandamizi kutoka ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, Salma Saleh amesema mfumuko huo uliongezeka kutokana na kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo kilikuwa na mahitaji muhimu ya chakula pamoja na bidhaa za mazao.

Bi Salma Saleh amesema bidhaa za vyakula ambavyo vingi vinatoka Tanzania bara bei yake ilipanda kwa asilimia 6.9 na hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wananchi ambao wengi walikua wakihitaji bidhaa hiyo.

Ofisa huyo aliziorodhesha bidhaa hizo zilizopanda ni pamoja na mchele aina ya mapembe,mchele kutoka Tanzania bara ikiwemo Mbeya, Unga wa ngano pamoja na sukari bei yake ilipanda kutokana na bidhaa hizo kuagizwa kutoka nje ya nchi.