Jumatatu , 26th Sep , 2022

Maandamano ya kuipinga serikali yanafanyika katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Tunisia, Tunis. 

Waandamanaji wanaukosoa utawala wa Rais Kais Saied kwa kushindwa kukabiliana na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za bidhaa muhimu. 

Waandamanaji wengi wameonekana katika wilaya ya Douar Hicher huku wakiwa kwenye maduka makuu kulalamikia ukubwa wa bei za bidhaa hawa chakula. Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji ambao walifunga barabara kwa kutumia mawe na kuwarushia mawe maaskari .

Waandamanaji hao wana hasira  baada ya mtu mmoja kujiua kufuatia madai ya kunyanyaswa na askari wa jiji kwa kosa la kufanya umachinga katika eneo ambalo halijaruhusiwa.