Alhamisi , 14th Apr , 2022

Katika hali isiyo ya kawaida Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi ameoneka akiwa na furaha ya hali ya juu wakati akiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mwanza.

Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi na wafuasi wake wakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza

Mfalme Zumaridi amewasili mahakamani hapo akiwa  amejiremba licha ya wafuasi wake walioapa kubaki naye  gerezani wakiendelea kupukutika na hadi kufikia leo wakiwa wamebaki watano pekee kati ya 93.

Zumaridi na wafuasi wake 93 wanakabili na kesi tatu 10, 11 na 12 zote za mwaka 2022 na katika kesi namba 10 ya usafirishaji haramu wa binadamu inamkabili Zumaridi peke yake ambapo wakili wa serikali Emmanuel Luvinga amesema upelezi wake bado haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ya kusomwa.

Wakili wa serikali Emmanuel Luvinga ameiambia mahakama hiyo kuwa kesi namba 11 na namba 12 ambazo zinamkabili Zumaridi na wafuasi wake upelelezi wake umekamilika lakini kutokana na hakimu anayesimamia kesi hizo kutokuwepo mahakamani akaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine atakapokuwepo hakimu huyo ili maelezo ya awali yasomwe.

Kesi hiyo imeendeshwa na hakimu mkazi Stella Kiama wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza ambapo imepangwa tena hadi Aprili 28, huku washtakiwa ambao hawajadhaminiwa hadi sasa akiwemo na Zumaridi wakirudishwa rumande katika gereza kuu la Butimba na waliopo nje kwa dhamana wakitakiwa kuripoti mahakamani hapo siku ya tarehe 28 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Unaweza kutazama video ya kilichojiri mahakamani hapo