Jumapili , 8th Oct , 2023

Madaktari wameeleza kuwa moja ya changamioto wanazokutana nazo hasa katika uchunguzi wa afya za watoto ni pamoja na kukutana na mabaki ya  vitu kama maharagwe, mende na pamba masikioni.

Mende

Wameeleza kuwa licha ya changamoto hizo pia yapo mambo mengine ikiwemo uzito mkubwa na mdogo , maambukizi katika koo,uoni hafifu na usikivu hafifu

Akitoa maelezo hayo jijini Dodoma Daktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa yya Muhimbili, Namala Mkopi alisema changamoto hizo kwa watoto kuingiza vitu masikioni  wamekuwa wakikutana nazo pindi watoto wanapowafanyia watoto uchunguzi.

Amesema watoto hao huviingiza vitu hivyo masikioni wanapokuwa katika michezo na huwawia vigumu wazazi kubaini hadi pale madhara yanapotokea na kuwa makubwa zaidi.

''Mfano mtoto akiweka pamba sikioni ikaakaa kwa mda mrefu kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi, kwani sikio linashindwa kujisafisha vizuri, usaha unajitengeneza na kutengeneza bakteria''- alisema

Dkt. Mkopi anayetoka Chama cha Madaktari wa watoto Tanzania (PAT) alisema hali hiyo endapo itampata mtoto ambaye bado hajaanza kuongea asipoatiwa matibabu inaweza kumsababishia apoteze uwezo wa kuongea.

Alisema japo wazazi wengi wananwaona watoto wao ni wazim a ni vyema wawe wanawapeleka hospitalini mara kwa mara kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini changamoto hizo na zikatatuliwa mapema kuliko kuziacha zikaendelea na kuja kuwa tatizo kubwa.

Kufuatia umuhimu wa uchunguzi kwa afya za watoto (PAT) kwa kushirikiana na shirika la kikikristo la Huduma za Jamii(CSSC) na Taasisi ya Stuft Africa< wameanzisha Program Maalum ya uchunguzi kwa wanafunzi.

Akieleza hilo mshauri wa huduma za elimu wa CSSC , Joshua Moshi alisema lengo ni kufanya uchunguzi kwa wanafunzi wote nchini ili waweze kujifunza vizuri.

Naye mratibu wa program hiyo Kutoka Taasisi ya STUFT Africa Helen Achimponta alisema lengo lao ni kugundua changamoto za kiafya za watoto zikiwa katika hatua za awali ili kuwatibu.

''Lengo lingine nikuwashauri waweze kuwasaidia watoto waweze kufanya vizuri zaidi shuleni''- alisema 

Naye ofisa elimu wa kata ya Mnadani Robert Tesha aliishauri serikali kuweka mpango utakaowezesha timu ya madaktari kupita katika shule kila muhula ili kuwafanyia uchunguzi wanafunzi.