Jumaa Aweso, Mbunge wa Pangani
Mbunge wa Jimbo la Pangani, Jumaa Aweso aliyeshiriki kipindi cha Weekend Breakfast siku ya Jumapili, ameiomba serikali kuchukua hatua za haraka na kuharakisha mchakato wa ajira za walimu kumaliza tatizo hilo kwa kuwa kuna baadhi ya shule wanafunzi hawana kabisa walimu.
Kuhusu walimu wa masomo ya sanaa, Aweso ambaye anaendelsha kampeni ya kuhamasisha elimu wilayani humo ijulikanayo kama 'Niaje Nisome Pangani inanitegemea', amesema walimu wa masomo hayo wapo wa kutosha na kwamba kipaumbele chao kama halmashauri kwa sasa ni ELIMU, ELIMU, ELIMU.
Mtazame hapa akielezea zaidi.........